Wameshindwa kutwaa ubingwa wakihitaji alama Moja kwenye michezo minne


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

"Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni". Hivyo ndivyo inavyoweza kuelezea kilichotokea katika mbio za ubingwa wa China Super League msimu wa 2026, baada ya klabu ya Chengdu Rongcheng kushindwa kutwaa taji wakati ambapo Kila mmoja aliamini waenda kutwaa taji hilo na kuandika historia ya soka katika Ligi hiyo.

Ikiwa imesalia michezo mitano kabla ya msimu kumalizika, Chengdu ilikuwa ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama14 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Dalian Yingbo. Wakati huo, timu hiyo ilikuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa ligi hiyo, huku ikihitaji alama moja pekee katika michezo minne iliyokuwa imesalia.


Hata hivyo, mambo yalibadilika katika michezo ya mwisho ambapo klabu ya Chengdu ilipoteza michezo yake minne ya mwisho na kushindwa kuvuna Ile alama Moja ambayo ingewapa nafasi ya kutwaa ubingwa huku wakati huo klabu ya Dalian Yingbo ikishinda michezo yake mitano ya mwisho na kupindua meza kibabe na kutwaa ubingwa.

Baada ya michezo hiyo, timu zote mbili zilimaliza ligi zikiwa na alama 52, lakini Dalian Yingbo ikatangazwa bingwa licha ya kuwa na tofauti ndogo ya kufunga na kufungwa.

Hii inatokana na kanuni za China Super League ambazo, timu zinapomaliza ligi zikiwa na alama sawa, Cha kwanza kuangaliwa ni matokeo ya michezo ya ana kwa ana kati ya timu hizo kabla ya kuangalia tofauti ya mabao ya jumla.


Katika michezo miwili ya ligi kati ya Chengdu na Dalian, Dalian ilishinda yote, hivyo kupata alama sita dhidi ya Chengdu, jambo lililoipa nafasi ya kutwaa ubingwa.

Kwa takwimu za jumla, Dalian ilikuwa na tofauti ya mabao matano (+5), wakati Chengdu ilikuwa na tofauti ya mabao 15 (+15). Hata hivyo, tofauti hiyo haikusaidia Chengdu kutokana na kanuni za ligi hiyo.

Hivyo, Dalian Yingbo imetwaa ubingwa wake wa kwanza wa China Super League, huku Chengdu Rongcheng ikimaliza katika nafasi ya pili baada ya kushindwa kutumia nafasi iliyokuwa nayo kuelekea mwisho wa msimu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments