Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo wa fainali Ngao ya jamii ligi kuu wanawake Tanzania Bara itawakutanisha Simba queens dhidi ya JKTqueens siku ya octoba 12 mwaka huu katika dimba la KMC Complex ambapo kutaakuwa na michezo miwili , mshindi wa tatu na fainali.
Mchezo wa mshindi wa tatu utapigwa saa 6:00 mchana ambapo Yanga princess watamenyana na Mashujaa Queens, huku Saa 9:00 fainali ndio utapigwa kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi hiyo.
Katika michezo ya nusu fainali Yanga na JKT walitoahana sare ya 1-1 dakika tisini lakini mikwaju ya penati iliwapeleka JKT fainali kwa ushindi wa 6-5, huku Simba wakiiburuza Mashujaa ndani ya dakika tisini kwa ushindi wa 2-0.
Fainali inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na ubora wa timu zote mbili ukizingatia JKT ndiye bingwa mtetezi wa ligi hiyo huku klabu ya Simba wanawake wakiwa wamesahijili vizuri ,dakika tisini zitaamua ni nani atauanza msimu na kikombe liguu wanawake Tanzania Bara.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment