Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hatua ya pili ya Awali ya mashindano ya Klabu bingwa na shirikisho barani Africa ipo wazi kwa Kila timu iliyo fuzu imekwisha mfahamu mpinzani wake, hatua hii inatarajiwa kuanza kutimua vumbi October 18/25 kwa mzunguko wa kwanza na wapili.
Timu tano zilizofuzu kutoka Tanzania zinaonekana kwenda kuandika historia ya kipekee ambapo nne kati Yao zinanafasi ya kufuzu makundi baada ya Azam kupaangwa na KMKM ya Zanzibar ,kama timu hizi zikicheza kwa kujitoa hakuna mpinzani wa kutisha kati yao japo mpira ni mchezo wa dakika 90, ila ikiwa karata zitachangwa vyema Klabu zote nne zitakwenda hatua ya makundi.
Katika hatua hiyo klabu za Simba, Yanga na Azam zitaanzia ugenini huku Singida black stars wakianzia nyumbani, kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa Yanga watamenyana na Silver Striker kutoka nchini Malawi, Simba dhidi ya Nsingizin Hotspurs ya Eswatini, Azam dhidi ya KMKM kutoka Visiwani Zanzibar na Singida wataanzia nyumbani dhidi ya Flambeau kutoka Burundi.
Nafasi ya timu hizi kutoka Tanzania kuingia hatua ya makundi ipo kubwa na hii itakwenda kuonyesha ni kwa kiasi gani soka letu linazidi kukua zaidi na zaidi Cha muhimu kwa timu hizi ni kuchanga karata zao vizuri ili kufika mbali zaidi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com
Post a Comment