Ubingwa wa Epl, Uefa wazipa mzuka Arsenal na PSG


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kumi wa Ligi Kuu England, mbio za kuwania ubingwa zimeanza kutoa taswira kwa timu zinazoweza kushindana kwa karibu, huku Arsenal ikionekana kuwa na nafasi ya kutetea taji lake.

Baada ya mzunguko huo, Arsenal inaendelea kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 27, ikiwa mbele kwa alama tano dhidi ya mpinzani wake wa karibu Brighton mwenye alama 22 huku nafasi ya tatu akiwa Manchester City, na alama 21.

Ikumbukwe kuwa The Gunners ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo baada ya kutwaa taji la msimu wa 2025/26, kwa mara ya kwanza baada ya takribani miongo miwili. Katika msimu huo, pia walifanikiwa kufika fainali ya UEFA Champions League, ingawa walipoteza kwa mikwaju ya penalti.


Baada ya kurejea kwenye kilele cha soka la England, Arsenal imeendelea na mwenendo mzuri katika msimu wa 2026/27 huku Ushindi katika michezo ya awali ya ligi umeifanya timu hiyo kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa, huku wapinzani wake wakipoteza alama muhimu.

Mwenendo huo unaweza kulinganishwa na Paris Saint-Germain (PSG) katika UEFA Champions League ambapo Klabu hiyo ya Ufaransa ilitwaa taji lake la kwanza mwaka 2025, kabla ya kulirudia mwaka 2026 na kuendelea kuwa miongoni mwa timu zinazowania ubingwa.

Hivyo, Arsenal inaweza kufuata mkondo huo kwa kuendeleza mafanikio yake baada ya kutwaa ubingwa wa msimu uliopita, hata hivyo, safari ya ligi bado ni ndefu na mwenendo wa timu nyingine unaweza kubadilisha hali ya ushindani katika mizunguko ijayo.


Mwenendo wa Arsenal baada ya kutwaa taji la ligi kuu baada ya takribani miaka 20 ya ukame umetoa chachu kwa klabu hiyo kuendelea kufanya vizuri huku ikiwa ni timu inayopewa nafasi ya kutetea ubingwa waio, huku Kwa upande wa PSG ikitwa timu tishio kwa upande wa uefa baada ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza ndio imekuwa chachu ya kuendelea kufanya vizuri wakitwaa taji hilo mara mbili mfululizo na mwaka huu ikiwa ni miongoni mwa klabu zinazo pewa nafasi ya kufanya vizuri.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments