Tetesi: Madrid, United kuwania Saini ya Staa Ulaya


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu za Real Madrid na Manchester United zimeanza kuhusishwa na mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Nico Paz, anayekipiga katika klabu ya Como ya Italia.

Taarifa zinaeleza kuwa Manchester United inaifuatilia hali ya mchezaji huyo na huenda ikatoa ofa ya kumsajili endapo atakuwa tayari kujiunga na klabu hiyo ya England.

Hata hivyo, Real Madrid nayo imeanza kujadili uwezekano wa kumrejesha mchezaji huyo Santiago Bernabeu, huku mazungumzo ya awali yakihusisha wawakilishi wake pamoja na watu wa karibu na mchezaji huyo.


Nico Paz mwenye umri wa miaka 22 aliwahi kuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid kabla ya kujiunga na Como, ambako ameendelea kuwasha moto kupitia kiwango chake.

Hadi sasa, haijathibitishwa ni klabu gani itakayofanikiwa kupata saini ya kiungo huyo, huku Real Madrid na Manchester United zikihusishwa na mpango wa kumhitaji nyota huyo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments