Tetesi: Doumbia hatarini kukosa nafasi Msimbazi


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Uongozi wa klabu ya Simba SC unatajwa kuelekeza nguvu katika usajili wa mshambuliaji Prince Dube mwezi January, hatua inayoweza kuongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji na kuiweka nafasi ya Ibrahim Doumbia kwenye changamoto ya kuendelea kupata nafasi ndani ya kikosi hicho.

Doumbia ambaye amejiunga na Simba akitokea nchini Mali, hajafanikiwa kuonyesha uwezo wa kufunga mabao kwa kiwango kilichotarajiwa, akiwa amefunga mabao mawili tangu alipojiunga na klabu hiyo.

Taarifa za Simba kuhitaji huduma ya Dube zinakuja wakati klabu hiyo ikijiandaa na hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako inahitaji kuwa na safu ya ushambuliaji yenye uwezo wa kutumia nafasi zinazotengenezwa huku Dube akionekana kuwa mmoja wa wakombozi kwenye upande huo.


Iwapo Simba itafanikiwa kufikia makubaliano ya kumsajili Dube, ambaye kwa sasa anaitumikia Hardrock FC ya Zimbabwe baada ya kuondoka Yanga, hilo linaweza kutatua changamoto ya upachikaji mabao inayo wakumba wekundu wa msimbazi kutokana na ubora wa mchezaji huyo alio uonyesha nchini akiwa kwenye klabu za Azam na Yanga.

Hata hivyo, usajili wa Dube pekee hautakuwa suluhisho la changamoto ya ufungaji mabao, kwani mchango wake utategemea kiwango atakachoonyesha, utimamu wa mwili na namna atakavyoweza kuendana na mfumo wa timu.

Kwa upande wa Doumbia, hatua hiyo inaweza kuwa changamoto baada ya klabu Kuona hatoshi na kuamua kutafuta mbadala, huenda klabu ikafanya maamuzi ya kumtoa kwa mkopo mwezi January au kumuuza iwapo watafanikiwa kufanya usajili wa mshambuliaji mwingine.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments