Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 ( Serengeti boys) imeanza mashindano ya kombe la Dunia ngazi ya vijana inayofanyika nchini Quatar baada ya kupata sare ya 2-2 dhidi ya Costa Rica kwenye mchezo wa kwanza kundi I.
Baada ya matokeo hayo , vijana hao wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama Moja , nafasi ya pili Costa Rica alama Moja huku Brazili akiongoza na alama tatu na anae buruza mkia ni Ireland ambaye hana alama.
Katika mashindano hayo Kuna Jumla ya makundi 12, huku Kila kundi likitakiwa kutoa timu mbili huku timu nane zikipatikana kwa njia ya best looser ambazo ni timu zitakazo shika nafasi ya tatu kwa idadi nzuri ya alama huku Serengeti boys wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa timu zinazoshika nafasi ya tatu na alama nzuri.
Hii ni taa ya kijani kwa vijana hao kwani wameonyesha kiwango kizuri kinacho shawishi kusema watafika hatua za juu kwenye mashindano hayo.
Mchezo unaofuata utapigwa novemba 24 dhidi ya Brazili huku karata ya mwisho ikihitimishwa novemba 27, dhidi ya Ireland.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment