Rekodi ya dakika 9 imevunjwa kwa dakika nane ligi ya mabingwa Ulaya


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imeweka rekodi mpya katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga mabao manne ndani ya dakika nane katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Villarreal.

Katika mchezo huo, Joao Neves alianza kuifungia PSG dakika ya tisa, kabla ya Desire Doue kuongeza bao la pili dakika ya 12 huku Senny Mayulu akifunga bao la tatu dakika ya 13, na Fabian Ruiz akihitimisha mfululizo huo kwa bao la nne dakika ya 17.


Kwa kufanya hivyo, PSG imevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Shakhtar Donetsk ya Ukraine, ambayo mwaka 2014 iliifunga BATE Borisov mabao 7-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo, Shakhtar ilifunga mabao manne ndani ya dakika tisa na sekunde 22, rekodi iliyodumu kwa miaka 12 kabla ya PSG kuivunja kwa kutumia dakika saba na sekunde 35 pekee.

Rekodi hiyo inaifanya PSG kuingia katika historia ya mashindano hayo, huku ushindi wake dhidi ya Villarreal ukiwa sehemu nyingine ya kumbukumbu ya klabu hiyo katika soka la Ulaya.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments