Timothy Lugembe
Mwanakwetusports.
Rais wa klabu ya Young Africans, Eng. Hersi Said, amesema klabu hiyo inaendelea kufungua milango kwa vijana wake kupata fursa za kwenda kucheza soka nje ya nchi, ikiwa ni sehemu ya kuwajengea mazingira ya kukuza vipaji vyao.
Kauli hiyo inakuja baada ya kiungo kijana wa klabu hiyo, Juma Issa Abushiri, maarufu kama ‘Chuga Boy’, kupata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Palmeiras inayoshiriki Ligi Kuu nchini Brazil.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Yanga SC inaendelea na taratibu za kumpatia mchezaji huyo VISA ili aweze kusafiri kwenda Brazil kwa ajili ya majaribio hayo.
Iwapo atafanya vizuri na kufikia vigezo vinavyohitajika, Abushiri anaweza kupata nafasi ya kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Hii inakuwa neema kwa vijana wa kitanzania kwani hapo awali nyota kadhaa walikuja kukipiga ligi kuu Tanzania bara wakitokea Brazil, mfano ni Coutinho na Jaja waliowahi kukipiga kwenye klabu ya Yanga, safari hii ni zamu ya Chuga boy kuipeperusha bendela ya Taifa nchini Brazil.
Hatua hii ni chachu kwa vijana wanao sakata kabumbu nchini kuelewa kuwa kazi wanayo ifanya inaonekana sehemu mbali mbali Duniani, hivyo wanatakiwa kuongeza juhudi ili kupata ofa zaidi ya kukipiga nje ya Tanzania hususani kwenye mataifa yaliyonendelea kwenye soka.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment