Nyota wa Singida akacha timu na uraia wa Tanzania


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo wa Singida black stars Mohamed Damaro Camara, ametangaza rasmi uamuzi wa kuachana na uraia wa Tanzania alioupata kupitia utaratibu wa uraia wa kujiandikisha kwaajili ya kulitumikia soka kama mtanzania.

Damaro, raia wa Guinea, ameeleza kuwa uamuzi huo umechangiwa na changamoto za masuala yanayohusu familia yake, akibainisha kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kupitia hali mbalimbali katika maisha yake.

Kupitia ujumbe wake, mchezaji huyo amewaomba mashabiki na Watanzania kwa ujumla kuelewa uamuzi wake, akisisitiza kuwa umefikiwa kutokana na sababu zake binafsi .

Kwa upande wa soka, Damaro ameeleza pia kusitisha mkataba wake na Singida Black Stars inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania, huku akitoa shukrani kwa viongozi wa klabu hiyo, mashabiki na wadau wote wa soka kwa ushirikiano waliompa katika kipindi alichokuwa sehemu ya timu hiyo.

Uamuzi huo unahitimisha pia ukurasa wa Damaro katika safari yake ya soka nchini Tanzania, ambako aliwahi kuitumikia Yanga kabla ya kujiunga na Singida Black Stars.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments