Novemba 3 yaacha simanzi kwenye familia ya Soka


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa CD Tenerife, Jesus de Miguel (30), amefariki dunia baada ya kupata ajali ya kugongana na kipa wa FC Andorra, Jesus Owono, wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la Pili nchini Hispania uliopigwa novemba 2, 2026.

Tukio hilo lilitokea baada ya Owono kutoka golini kuwania mpira na isivyo bahati aligongana na De Miguel, hali iliyosababisha mshambuliaji huyo kuanguka chini akiwa amepoteza fahamu.

Baada ya tukio hilo, De Miguel alipewa huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa hospital kwa matibabu zaidi, hata hivyo, juhudi za kumuokoa hazikufanikiwa na ilipofika novemba 3, 2026 nyota huyo alifariki Dunia.

Kwa upande wa Owono, tukio hilo lilimwacha akiwa katika hali ya huzuni kutokana na kile kilichotokea uwanjani.

Matukio kama haya yanawakumbusha wanamichezo kulinda usalama wa Kila mmoja wapo wapo uwanjani, kwa kufanya hivyo kutapunguza hatari ya wachezaji kupata ukilema wa milele na hata kuondoka uwezekano wa mchezaji kupoteza maisha.

Pumzika kwa amani shujaa katika soka.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments