Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ushindani wa Simba na Yanga umeshuhudia wachezaji wakihama kutoka klabu moja kwenda nyingine, lakini imekuwa adimu kusikia kocha akihamia upande wa pili. Lakini hali ya kocha kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili imehitokeza mara mbili.
Miongoni mwa makocha hao ni marehemu Syllersaid Salmin Kahema Mziray, ambaye alianza kuifundisha Simba mwaka 1990 akishirikiana na Abdallah Kibadeni.
Baada ya kuondoka Simba, mwaka 1991 alijiunga rasmi na Yanga na kuiongoza katika mashindano mbalimbali, ikiwemo fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Simba mwaka 1992, Mziray aliwahi pia kurejea Yanga mwaka 2004 kabla ya kufariki dunia mwaka 2010.
Kocha mwingine ni Fadlu Davids kutoka Afrika Kusini, ambaye aliiongoza Simba kuanzia mwaka 2024 na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) japo hakufanikiwa kutwaa ubingwa huo.
Baada ya kuondoka Simba, Davids aliendelea na kazi ya ukocha akiwa Raja Casablanca ya Morocco na sasa katangazwa kuwa kocha mkuu wa Yanga Novemba 7, 2026.
Hivyo, Mziray na Fadlu Davids ni miongoni mwa makocha waliowahi kufanya kazi katika klabu zote mbili zinazoshiriki ushindani mkubwa wa soka nchini Tanzania.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment