Maisha bila Messi yaanza na misuko suko timu ya Taifa


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Baada ya Lionel Messi kutundika daluga na kuhitimisha safari yake ya kuitumikia timu ya taifa ya Argentina, kikosi hicho kimeanza ukurasa mpya bila nahodha wake kwa kupoteza mchezo wake wa kwanza.

Argentina imekubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Uruguay katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Novemba 13, 2026, kwenye Uwanja wa La Bombonera.

Uruguay ilipata bao la kwanza kupitia Leonardo Balerdi aliyejifunga dakika ya 48, kabla ya Maximiliano Araujo kuongeza bao la pili dakika ya 53 huku Julian Alvarez aliifungia Argentina dakika ya 73, lakini haikutosha kuzuia kipigo hicho.


Ikumbukwe kuwa, kabla ya kipigo hicho, Argentina ilikuwa haijapoteza mchezo wowote ndani ya dakika 90 kwa kipindi cha siku 430, tangu ilipofungwa bao 1-0 na Ecuador Septemba 9, 2025, katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026. Hivyo, kipigo dhidi ya Uruguay kimekuwa Cha kwanza tangu kustaafu kwa Lionel Messi.

Kupoteza kwa Argentina katika mchezo wake wa kwanza baada ya Messi kuhitimisha safari yake ya timu ya taifa kunafungua mjadala kuhusu namna kikosi hicho kitakavyoendelea bila mchezaji aliyekuwa sehemu ya mafanikio yake kwa miaka mingi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments