Kumi za msimu jana na msimu huu zatengeneza rekodi Msimbazi


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba imeendelea kuonyesha mwendelezo mzuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa na lengo la kurejesha taji la ligi ambalo imekosa kwa muda mrefu, Safari hiyo imeambatana na rekodi mbalimbali zinazowekwa chini ya kocha wao, Steve Barker, raia wa Afrika Kusini.

Mnyama amefikisha michezo 20 mfululizo ya ligi bila kupoteza alama, akishinda michezo yote , Katika msimu wa 2026/27, Simba imeshinda michezo 10 ya mwanzo na kukusanya alama 30, ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Michezo hiyo 10 imeungana na ushindi 10 wa mwisho wa msimu wa 2025/26, na kufanya Simba kufikisha ushindi 20 mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mwendelezo huo umeiweka Simba katika historia ya ligi hiyo, huku pia ikiipiku rekodi ya FC Bayern Munich ya ushindi 19 mfululizo katika Bundesliga ya Ujerumani, iliyowekwa msimu wa 2013/14.


Hatua hiyo imekamilishwa baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC, Novemba 2, 2026, na kufikisha ushindi wake wa 20 mfululizo.

Hata hivyo, safari ya Simba bado inaendelea Kadri michezo ya ligi inavyoendelea, timu hiyo ina nafasi ya kuongeza idadi ya ushindi huo, huku kila mchezo ukiwa sehemu ya historia inayojengwa na kikosi cha Barker.

Ushindi 10 ya mwisho wa msimu uliopita na ushindi 10 ya mwanzo wa msimu huu ndiyo umeunda rekodi hiyo ya michezo 20 mfululizo kwa Wekundu wa Msimbazi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments