Kifo Chamuweka Owono kwenye hati hati za kutundika daruga


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Goli Kipa wa klabu ya FC Andorra, Jesus Owono, anaripotiwa kufikiria kustaafu soka siku chache baada ya tukio la ajali uwanjani lililosababisha kifo cha mshambuliaji wa CD Tenerife, Jesus de Miguel kilichotokea novemba 3, 2026.

Tukio hilo limemuathiri Owono na kufikiria kuachana na soka akiwa na miaka 25, hata hivyo klabu yake imemtafutia msaada wa kisaikolijia ili kuhakikisha nyota huyo anarudi kwenye hali yake ya kawaida na kuendelea kusakata kandanda badala ya kufikiria kutundika daruga.

Katika jitihada za kuendelea kumuweka sawa nyota huyo, klabu ya FC Andorra inajaribu kumsaidia kurejea katika hali yake ya kawaida kwa kumweleza kuhusu matukio mengine yanayofanana na hilo yaliyowahi kutokea katika soka na namna wachezaji waliohusika kabiliana na hali hiyo.

Kutokana na athari za tukio hilo, Owono bado anahitaji msaada wa kisaikolojia kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake katika soka.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments