Jj Gabriel kuiacha United, Kutimkia Real Madrid


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezaji chipukizi mwenye umri wa miaka 16, JJ Gabriel, anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Manchester United na kujiunga na Real Madrid ya Hispania.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Gabriel amethibitisha uamuzi wa kuondoka Manchester United na tayari ametoa ishara ya kuaga klabu hiyo huku akielekea kuanza maisha mapya na klabu ya Real Madrid.

Inaelezwa kuwa makubaliano ya uhamisho huo yamefikia hatua za mwisho, huku pande husika zikisubiri kukamilisha taratibu za kusaini mkataba.

Kinda huyo amefikia maamuzi hayo baada ya klabu ya United kushindwa kutimiza masharti yake ikiwemo angalau kupata dakika kadhaa kwenye michezo inayo husisha timu ya wakubwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com





0/Post a Comment/Comments