Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Nyota wa timu ya Taifa ya Misri Mohamed Salah ameandika rekodi mpya katika soka la nchi hiyo baada ya kufikisha mabao 70 katika timu ya taifa, akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Hossam Hassan.
Rasmi nyota huyo ndiye mfalme mpya wa mafarao katika upachikaji wa mabao baada ya kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa.
Salah alifikia hatua hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Malawi, mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 uliochezwa Novemba 13, 2026, jijini Cairo.
Mabao hayo aliyafunga katika dakika ya 84 na 90+5 , na kufikisha jumla ya mabao 70 katika michezo 123 ya timu ya taifa.
Kwa kufanya hivyo, Salah amempita Hossam Hassan aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo kwa mabao 69, na sasa anakuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya timu ya taifa ya Misri.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment