fainali iliyopigwa kwa takribani miezi kumi yatamatika novemba 24


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Senegal (Simba wa Teranga) wametangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kutoa uamuzi wa mwisho na kurejesha ushindi wao wa mabao 1-0 dhidi ya Morocco.

Uamuzi huo umetolewa Novemba 24, 2026, baada ya sintofahamu ya muda mrefu kuhusu nani anayestahili kuwa bingwa wa mashindano hayo.

Fainali hiyo iliyopigwa Januari 18, 2026, katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat, Morocco, ilikuwa na mvutano mkubwa kutokana na ushindani wa timu hizo mbili ambazo ni miongoni mwa timu zilizokuwa zikipewa nafasi ya kutwaa ubingwa.

Mchezo huo ulikuwa wa vuta ni kuvute, huku timu zote zikishindwa kupata bao katika muda wa kawaida wa dakika 90.

Hata hivyo, dakika ya 90+8, Morocco walipata mkwaju wa penalti wenye utata, jambo lililosababisha wachezaji wa Senegal kususia mchezo na kwenda vyumbani wakipinga uamuzi huo.

Baada ya kusimama kwa mchezo kwa takribani dakika 14, wachezaji wa Senegal walirejea uwanjani na kukubali mchezo kuendelea uku mchezaji wa Morocco, Brahim Diaz, alikosa mkwaju huo wa penalti, na mchezo kuingia dakika za nyongeza.


Dakika ya 93 kwenye muda wa nyongeza , Senegal walipata bao kupitia Pape Gueye, lililowapa ushindi wa mabao 1-0 na kutwaa ubingwa wa AFCON 2025.

Baada ya matokeo hayo, Morocco waliwasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wakipinga mwenendo wa mchezo, hasa kitendo cha wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika.

Machi 2026, Bodi ya Rufaa ya CAF iliamua kuwa Senegal wamepoteza mchezo kwa kutoendelea kucheza, na kuipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3-0.

Hata hivyo, Senegal hawakukubaliana na uamuzi huo, wakakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), wakitaka matokeo ya uwanjani kurejeshwa.


Hatimaye, Novemba 24, 2026, CAS imetengua uamuzi wa Bodi ya Rufaa ya CAF na kurejesha matokeo ya awali ya fainali hiyo, hivyo kuthibitisha ushindi wa Senegal wa mabao 1-0.

Kwa uamuzi huo, Simba wa Teranga wamehitimisha safari ya kisheria iliyochukua takribani miezi 10, na sasa Senegal ni mabingwa rasmi wa AFCON 2025.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments