Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Baada ya klabu ya Como kufanya vizuri katika Ligi kuu nchini Italy na mashindano ya Klabu bingwa barani Ulaya , klabu hiyo inapanga kuweka mfumo wa kiuchezaji ambao utawafanya kuzidi kulitawala soka la Ulaya.
Akitoa mtazamo huo, Rais wa klabu ya Como 1907, Mirwan Suwarso, ameeleza nia yake ya kuijenga timu hiyo kwa kufuata falsafa ya uchezaji inayofanana na Barcelona ya Hispania.
Suwarso anataka Como iwe na utambulisho wa soka unaozingatia kumiliki mpira, kufanya pressing ya juu na kucheza soka la kushambulia badala ya kutegemea matokeo pekee.
Mtazamo huo unaonesha kuwa uongozi wa Como unataka kujenga mfumo wa uchezaji utakaotambulika ndani na nje ya Italia, huku ukizingatia maendeleo ya timu kwa muda mrefu.
Barcelona imekuwa moja ya mifano ya soka linalojengwa katika umiliki wa mpira na matumizi ya pasi nyingi, falsafa ambayo Suwarso anatamani kuiona katika kikosi cha Como.
0767915463,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment