Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya AC Milan imefanikiwa kushinda dabi tatu mfululizo za ligi dhidi ya wapinzani wao Inter Milan kwa mara nyingine tangu mwaka 2004.
Milan imeweka rekodi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Inter katika dabi iliyochezwa Oktoba 31, 2026, matokeo yaliyowafanya kufikisha ushindi wa tatu mfululizo katika Serie A dhidi ya mahasimu wao.
Mara ya mwisho Milan kufanya hivyo ilikuwa mwaka 2004, wakati ilipokuwa chini ya kocha Carlo Ancelotti, ambapo ilifanikiwa kushinda dabi nne mfululizo za ligi dhidi ya Inter.
Ushindi huo pia umeiwezesha Milan kufikisha alama 21 na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi baada ya michezo 10, huku Inter ikiendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na alama 25.
Kwa upande wa kocha Ruben Amorim, ushindi huo unaendeleza mwenendo wa timu hiyo katika ligi, huku Milan ikirejea katika historia ya dabi kwa kuweka rekodi ambayo haikuwa imeifikia kwa zaidi ya miongo miwili.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment