Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Chelsea imepata pigo jingine kwenye kikosi chake baada ya mshambuliaji wao Joao Pedro kupata jeraha la paja linalotarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa wiki kadhaa.
Jeraha hilo limekuja wakati klabu hiyo ikiwa tayari inakabiliwa na changamoto ya majeraha ya wachezaji, akiwemo beki wake na nahodha Reece James.
Joao Pedro alipata jeraha hilo kabla ya mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur, hali inayomfanya akose baadhi ya michezo ya Chelsea katika kipindi kijacho.
Miongoni mwa michezo anayoweza kukosa ni dhidi ya Liverpool katika Kombe la Carabao na Manchester United katika Ligi Kuu England.
Kukosekana kwa mshambuliaji huyo ni changamoto kwa Chelsea kutokana na mchango wake katika safu ya ushambuliaji, hata hivyo, muda kamili wa kurejea kwake uwanjani bado haujathibitishwa.
0767915474,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment