United yavaa moyo wa chuma kwa Carrick


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Uongozi wa Manchester United umeamua kuendelea kumuamini kocha wake Michael Carrick licha ya matokeo ya timu hiyo katika michezo ya hivi karibuni ya msimu wa 2026/27.

United imekuwa na mwanzo usioridhisha wa msimu, hali iliyozua maswali kuhusu mustakabali wa Carrick na uwezekano wa kuondoka kwake kabla ya msimu kumalizika.

Katika michezo mitano iliyopita, Manchester United haijapata ushindi, ikiwa imepoteza mara tatu na kutoka sare mara mbili. Matokeo hayo yameifanya timu hiyo kubaki na alama saba na kushuka hadi nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi.

Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo umeamua kumpa Carrick nafasi nyingine ya kurekebisha hali ya timu na kuendelea kujenga kikosi kitakachoweza kupata matokeo ya ushindi.

Carrick anatarajiwa kuiongoza United katika mchezo ujao dhidi ya Chelsea, huku akiendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo.

Uamuzi huo unampa kocha nafasi ya kurekebisha mwenendo wake kwenye ligi, huku akitakiwa kutumia michezo inayofuata kuboresha matokeo na kuimarisha nafasi ya timu hiyo kwenye msimamo.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments