Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Manchester United bado haijapata ushindi
dhidi ya Atletico Madrid katika michezo mitano ya mashindano rasmi ambayo timu
hizo zimekutana, baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya Oktoba 13, 2026.
Historia yao ilianza mwaka 1991, ambapo Atletico
ilishinda mabao 3-0 katika Kombe la Washindi wa Vikombe Ulaya, mchezo wa
marudiano ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, hivyo Atlético kufuzu kwa jumla ya
mabao 4-1.
Timu hizo zilikutana tena katika hatua ya
16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2021/22. Mchezo wa kwanza uliisha
kwa sare ya bao 1-1, kabla ya Atletico kushinda bao 1-0 katika mchezo wa
marudiano uliochezwa Old Trafford.
Oktoba 13, 2026, Atletico iliendeleza
rekodi kwa kushinda mabao 2-0, Matokeo
hayo yanaifanya klabu hiyo ya Hispania kuwa na ushindi mara tatu na sare mbili
katika michezo hiyo mitano, huku Manchester United ikiwa bado haijapata ushindi
dhidi yake.
Kwa kuzingatia matokeo hayo, Atletico
Madrid imeendelea kuwa timu ambayo Manchester United haijaweza kuifunga katika
michezo Yao ya mashindano rasmi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment