Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Barcelona imeanza msimu wa 2026/2027 kwa kushinda mechi zake zote tisa za mashindano rasmi ya La Liga na UEFA Champions League, ikiwa na rekodi ya asilimia 100 ya ushindi.
Mabingwa hao wa Hispania wameendelea kupata matokeo mazuri katika michezo yao ya mwanzo, huku ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Getafe katika La Liga, Oktoba 10, 2026, ukiwa miongoni mwa matokeo yao ya hivi karibuni.
Rekodi hiyo ina maana kuwa katika mechi tisa zilizohesabiwa, Barcelona wameshinda zote bila kupoteza wala kutoka sare, huku wakiwa wamefunga mabao 39 na kuruhusu mabao nane.
Hata hivyo, msimu bado unaendelea na michezo bado ipo mingi, kwa mwenendo huu huenda wakatangaza ubingwa mapema ambapo kwa mzunguko nane ya laliga wapo kileleni kwa alama tano dhidi ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment