Traorè alivalia njuga suala la soka Burkina Faso


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré, amesema serikali yake itachukua hatua za moja kwa moja katika usimamizi wa soka nchini humo, ikiwa ni pamoja na kuingilia masuala yanayoweza kuisaidia sekta hiyo kuendelea.

Akizungumza kuhusu hatua hizo, Traoré amesema hawana chaguo zaidi ya kuendelea na mpango huo kwa lengo la kuboresha mipango na miundombinu, ili kuwasaidia wachezaji na kukuza mazingira bora ya soka nchini humo.


“Hatuna chaguo, inabidi tuingilie kati, bila kujali kama tutasimamishwa au la,” amesema Traore

Ameongeza kuwa serikali itatoa nafasi kwa watu wenye uwezo kutumia ujuzi wao kikamilifu, huku hatua hizo zikilenga kuifanya sekta ya michezo kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi.

Hata hivyo hatua hiyo inaweza kuibua mjadala kuhusu uhusiano kati ya serikali na uendeshaji wa soka, ikizingatiwa kuwa kuingiliwa kwa masuala ya soka na serikali kunaweza kuleta hatua za kinidhamu kutoka FIFA lakini Rais huyo amesema atafanya hivyo bila kujali suala hilo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments