Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC inatajwa kuhitaji huduma za kiungo wa Afrika Kusini, Asanele Velebayi, anayekipiga Kaizer Chiefs, katika hatua ya kuimarisha safu yake ya kiungo kwenye dirisha dogo la usajili.
Kocha wa Simba, Steve Barker, ameripotiwa kupendekeza jina la Velebayi kwa uongozi wa klabu hiyo ili liangaliwe katika mipango ya usajili.
Velebayi, mwenye umri wa miaka 23, ni kiungo anayeweza kucheza katikati ya uwanja na kusaidia timu katika kujenga mashambulizi, Uwezo wake wa kucheza nafasi hiyo unaweza kuwa miongoni mwa sababu zinazomfanya kuvutia benchi la ufundi la Simba.
Kwa sasa, kiungo huyo anakipiga Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini baada ya awali kuitumikia Cape Town , Pia amewahi kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini, jambo linaloonyesha kuwa amekuwa akifuatiliwa katika ngazi ya soka la kimataifa.
Endapo Simba itaamua kuendeleza mpango huo, uongozi wake utahitaji kufanya tathmini ya uwezekano wa kumpata mchezaji huyo pamoja na masharti ya usajili wake.
Hata hivyo, taarifa hizo ni tetesi bado uthibitisho rasmi kutoka kwa Simba SC au Kaizer Chiefs, hivyo haijathibitishwa kuwa mazungumzo ya usajili yameanza au klabu hizo zimefikia makubaliano.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment