Sharti la Olise kusini mkataba mpya Bayern


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Michael Olise, ameweka sharti katika mkataba wake mpya na klabu hiyo, akitaka kuwepo na kipengele Cha release clause kitakacho mruhusu kuondoka endapo klabu nyingine itafikia kiasi kilichowekwa.

Olise, ambaye awali aliichezea Crystal Palace, anaendelea kuhusishwa na mpango wa kusalia Bayern Munich kwa muda mrefu, huku wachezaji wengine kama Harry Kane na Jamal Musiala pia wakitajwa kuwa na vipengele kama hivyo kwenye mikataba yao.

Kinachozua mjadala Allianz Arena ni uwepo wa release clause hiyo, kwani ikitumika, Bayern haitakuwa na mamlaka ya kuzuia uhamisho endapo klabu inayomhitaji itafikia kiasi kilichowekwa na mchezaji akakubaliana na uhamisho huo.

Njia hii inampa nafasi mchezaji kufanya maamuzi endapo akihitaji kuanza maisha na klabu nyingine iwapo dau limefikiwa, huku Mtindo huu pia ukiwa unaipa klabu ugumu wa kumbakisha mchezaji muhimu wakati ambao Kuna timu inamuhitaji na imefikia kiwango huku mchezaji akiwa tayali kuondoka.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments