Sekunde 39 zinatosha kulipa faini ya Ronaldo


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Al Nassr na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, anakadiriwa kupata euro 6.61 kwa sekunde, kiasi kinachoonyesha ukubwa wa mshahara wake katika soka la kulipwa.

Kwa mujibu wa makadirio ya mshahara wake wa mwaka, Ronaldo analipwa takribani euro milioni 208.4 kwa mwaka akiwa na Al Nassr ya Saudi Arabia ambapo Kwa hesabu hiyo, faini ya euro 255 aliyopewa kama adhabu inalingana na mapato yake ya takribani sekunde 39.

Ulinganisho huo unaonyesha tofauti kati ya thamani ya faini na mapato yanayokadiriwa ya mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi duniani. Ingawa euro 255 ni kiasi kidogo ikilinganishwa na mshahara wake wa mwaka, umuhimu wa adhabu yoyote ya kinidhamu haupimwi kwa thamani ya fedha pekee, bali pia kwa sababu na athari zake kwa mchezaji.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo alipatiwa adhabu hiyo baada ya kuondoka kwenye kambi ya timu ya Taifa nchini Denmark wakati wa maandalizi ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Denmark 

Mbali na adhabu ya kifedha pia nyota huyo atalazimika kukaa nje ya timu ya Taifa kwa siku 30 kama sehemu ya adhabu nje ya kiasi Cha pesa.

Hivyo, adhabu hii ni kama kumkumbusha Ronaldo kuwa na nidhamu kwa viongozi wake ikiwemo benchi la Ufundi na sio kumfanya apate athari kutokana na makosa aliyo yafanya, kwani adhabu hiyo inaonekana ni ndogo ikilinganishwa na kipato chake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments