Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imeanza kujenga utawala wake katika mashindano ya UEFA Champions League baada ya kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo, hatua inayoiweka katika nafasi ya kuwania heshima ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikishikiliwa na Real Madrid.
PSG ilitwaa taji lake la kwanza la Champions League mwaka 2025 baada ya kuifunga Inter Milan mabao 5-0 katika mchezo wa fainali, kabla ya kuongeza taji la pili mwaka 2026 kwa kuwafunga Arsenal kwa mikwaju ya penati na kuendeleza mafanikio yake katika mashindano hayo.
Mafanikio hayo yanaifanya klabu hiyo ya Ufaransa kuingia katika kundi la timu zinazotajwa kuwania ubingwa kila msimu, hasa kutokana na uwezo wake wa kushindana na klabu zenye historia katika soka la Ulaya.
Kwa upande mwingine, Real Madrid inaendelea kuongoza kwa idadi ya mataji ya Champions League ikiwa na jumla ya vikombe 15, rekodi iliyoiweka katika nafasi ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo huku mara ya mwisho klabu hiyo kutwaa ubingwa ikiwa ni 2024 wakiifunga Dortmund 2-0.
Kwa miaka mingi, kukutana na Real Madrid katika Champions League kumekuwa changamoto kwa wapinzani wake kutokana na uzoefu wake katika mashindano hayo na uwezo wa kupata matokeo katika michezo yenye ushindani mkubwa.
Hata hivyo, PSG imeanza kuonyesha dalili za kutaka kujiweka katika nafasi hiyo baada ya kutwaa mataji mawili mfululizo, huku ikionyesha uwezo wa kushindana na baadhi ya vigogo wa soka la Ulaya.
Katika mchezo ya UEFA hatua ya Ligue phase PSG imepata ushindi katika michezo yote mitatu waliyocheza wameshinda yote kwakiifunga slovania batslava 6-1, huku vigogo wa Ulaya Manchester city na Barcelona nao wakikutana na kadhia ya kufungwa 4-2 Kila mmoja. matokeo hayo yanadhihirisha uwezo wao wa kushindana na timu zilizokuwa zikitajwa miongoni mwa wagombea wa ubingwa.
Ushindi huo ni sehemu ya safari ya PSG katika kujenga jina lake kwenye mashindano hayo, ingawa kufikia rekodi ya Real Madrid kunahitaji kuongeza mataji kwa misimu mingi ijayo.
Real Madrid yenyewe iliweka historia kwa kutwaa mataji matatu mfululizo ya Champions League kati ya mwaka 2016 , 2017 na 2018, mafanikio yanayoonyesha ukubwa wa kazi inayomkabili PSG ikiwa inataka kufikia kiwango hicho.
Kwa sasa, Real Madrid bado ni kinara wa Champions League kwa idadi ya mataji, lakini PSG imeanza kujenga hoja ya kuwa miongoni mwa timu zinazoweza kutawala mashindano hayo katika kipindi kijacho ikiwa itaendeleza mwenendo wake wa ubingwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment