Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha mkuu wa Bayern Munich, Vincent Kompany, amekimbizwa hospitali baada ya kuzimia alipokuwa akitazama mazoezi ya timu ya pili ya klabu hiyo siku ya October 23, 2026.
Taarifa ya Bayern Munich imesema Kompany alipata tatizo hilo akiwa uwanjani, kisha akapelekwa hospitalini kwa uchunguzi na matibabu.
Kwa mujibu wa klabu hiyo, kocha huyo anaendelea kufanyiwa uchunguzi na kubaki chini ya uangalizi wa madaktari ili kufuatilia hali yake.
Kutokana na tukio hilo, benchi la ufundi la Kompany litachukua majukumu ya kuongoza mazoezi na kusimamia timu siku za michezo hadi atakaporejea au klabu itakapotangaza utaratibu mwingine.
Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Max Eberl, amesema afya ya Kompany ni kipaumbele cha klabu hiyo na kwamba atapatiwa matibabu na msaada anaohitaji hadi atakapopata nafuu.
Hata hivyo, klabu hiyo haijataja chanzo cha kuzimia kwake wala muda anaotarajiwa kukaa hospitalini.
Bayern Munich imemtakia kocha huyo kupona haraka na imesema itaendelea kumpa muda na huduma anazohitaji.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment