Mnyama karibu kupata mrithi wa Zimbwe, Kapombe beki ya pembeni


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kwa zaidi ya misimu kumi, klabu ya Simba imekuwa na mabeki wa pembeni waliotumika katika kikosi cha klabu hiyo na timu ya Taifa, ambapo Mohamed Hussein akisimamia upande wa kushoto na Shomari Kapombe upande wa kulia.

Katika kipindi hicho, Simba ilisajili mabeki wengine wa ndani na kimataifa, lakini hakuna aliyefanikiwa kuwatoa moja kwa moja kwenye nafasi zao na kuwa chaguo la kwanza kwa muda mrefu.

Hali hiyo ilizua mjadala kuhusu nani angekuwa mrithi wa nyota hao, kutokana na kiwango kizuri walicho kionyesha mfululizo huku utimamu wa kimwili kwa kuhimili kutopata majeraha mara kwa mara ikiwa ni Moja ya upekee wa nyota hao.

Kwa sasa klabu ya Simba imesalia na Shomari Kapombe baada ya Mohamed Hussen kuondoka kwenye kikosi hicho na kujiunga na klabu ya Yanga Afrika.


Hata hivyo, mjadala wa upande wa kulia unaelekea kupata majibu baada ya Simba kumsajili Nathaniel Chilambo kutoka Azam FC. Usajili huo unampa kocha chaguo jingine katika nafasi hiyo, huku kiwango cha Chilambo kikimpa nafasi ya kuwania namba katika kikosi cha Msimbazi.

Ujio wake pia unaongeza ushindani katika nafasi hiyo, huku majeraha ya Kapombe yakimpa mchezaji huyo wakati mzuri wa kucheza na kuonyesha uwezo, kutokana na kiwango chake hakuna shaka kuwa Simba imepata mbadala wa Kapombe kwenye eneo hilo


Kwa upande wa kushoto, bado kuna swali kuhusu mrithi wa Mohamed Hussein, Mligo ni miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuwania nafasi hiyo, lakini bado anahitaji kuonyesha uwezo wa kumfanya kuwa chaguo la kudumu.

Hivyo, Simba inaonekana kuwa karibu kupata jibu upande wa kulia kupitia Chilambo, lakini upande wa kushoto bado unasubiri mwendelezo kutoka kwa nyota atakaye dhihirisha uwezo kwenye upande huo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments