Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kila Manchester United inapopitia kipindi kigumu, lawama zimekuwa zikielekezwa kwa uongozi wa klabu hiyo, hasa kuhusu namna unavyosimamia usajili na matumizi ya fedha.
Mjadala huo umeibuka baada ya United kupoteza dhidi ya Atlético Madrid katika mchezo wa UEFA Champions League ambapo beki wa kati wa klabu hiyo Lisandro Martínez ameingia kwenye mjadala huo kufuatia kauli kali dhidi ya uongozi wa klabu, akielekeza lawama kwa viongozi kwa kushindwa kutumia fedha ipasavyo katika usajili wa wachezaji jambo ambalo linakwamisha mafanikio ya timu.
Ikumbukwe kuwa Cristiano Ronaldo na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Ruben Amorim, pia waliwahi kuikosoa United kuhusu masuala ya uendeshaji na mwenendo wa timu hata hivyo baada ya ukosoaji wao hawakuwa tena sehemu ya timu
Sasa, Martínez naye anaweza kujikuta katika wakati mgumu kutokana na msimamo wake dhidi ya uongozi. Mkataba wake unakaribia kufikia mwaka wa mwisho, huku kukiwa na taarifa kwamba hataki kuongezewa mkataba na huenda akapendelea kuhamia Hispania.
Hali hiyo inaibua swali kuhusu mustakabali wa wachezaji na makocha wanaoikosoa klabu hiyo hadharani. Je, tatizo la Manchester United linatokana na watu walio ndani ya uwanja au maamuzi yanayofanywa nje ya uwanja?
Kwa miaka ya karibuni, mjadala kuhusu matumizi ya fedha katika usajili na uwezo wa uongozi kujenga timu yenye ushindani umeendelea kuikabili United, hivyo, badala ya kuishia kuwaondoa wanaoikosoa klabu, huenda suluhisho likawa kutathmini maamuzi yanayoifanya timu kushindwa kufikia matarajio yake.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment