Majibu ya vipimo yatuliza mioyo Fc Barcelona

  

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Baada ya vipimo kuhusu afya ya mshambuliaji wa Fc Barcelona Raphina, majibu yamekwenda vizuri baada ya vipimo kuonyesha kuwa hana Jeraha kubwa hivyo kuna uwezekano wa kuingia uwanjani kwenye mchezo unaofuata wa Laliga.

Raphinha aliondoka kwenye kambi ya Brazil baada ya kupata maumivu katika paja kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Australia uliomalizika kwa Brazil kushinda 4-2. 

Awali, vipimo vya Brazil vilionyesha uwepo wa uvimbe mdogo wa misuli katika sehemu ya nyuma ya paja la kulia, hali iliyosababisha kuondolewa kwenye kikosi kwa ajili ya mchezo dhidi ya India.

Hata hivyo, vipimo vipya alivyofanyiwa Barcelona vimeonyesha kuwa hana jeraha kubwa kiasi hicho, hivyo haarifa hiyo imeondoa hofu iliyokuwepo Barcelona kutokana na historia ya Raphinha kupata matatizo katika eneo hilo.

Kwa sasa, Raphinha anatarajiwa kuwa tayari kwa mchezo wa Barcelona dhidi ya Getafe utakaochezwa Oktoba 10, huku benchi la ufundi likiwa na nafasi ya kumpumzisha kama tahadhari.

Raphinha amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Barcelona msimu huu, akiwa amefunga mabao 14 katika mashindano yote, yakiwemo 12 kwenye LaLiga.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments