Kuitiwa polisi kwa kinda kwa geuka taa ya kijani kwenye soka


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Baada ya kuonyesha kiwango cha kipekee katika ligi ya soka iliyohusisha watoto wenye umri wa miaka mitano, Nevada Pierre, akiwa na miaka mitatu, ameonyesha umahiri wa kumiliki na kuuchezea mpira na kuwaacha baadhi ya watu midomo wazi.

Nevada, mtoto Mmarekani mwenye asili ya Afrika, alijikuta kwenye mgogoro uliosababisha polisi kuitwa uwanjani wakati wa mchezo huko Winter Park, Florida. Wazazi wake walidai kuwa mtoto wao alikuwa akiondolewa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa, huku mwandaaji wa ligi akieleza kuwa kulikuwa na malalamiko kuhusu tabia yake uwanjani huku Polisi wakieleza kuwa hakukuwa na kosa la jinai wala mtu aliyekamatwa.


Chanzo Cha sintofahamu hiyo ni baada ya mtoto kuonyesha kiwango Cha kipekee ndipo familia Moja ya kizungu wakaamua kuita polisi ili kumuondoa kijana huyo uwanjani wakidai alikaa na mpira kwa muda mrefu, huku kiwango chake kikiwa kikubwa kuliko watoto wengine.

Hata hivyo, tukio hilo limegeuka kuwa fursa nyingine kwa mtoto huyo baada ya Jay-Z, kupitia kampuni yake ya usimamizi wa wanamichezo ya Roc Nation Sports, kujitokeza kumuunga mkono.

Kampuni hiyo imeeleza kumuunga mkono Nevada na, kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, imepanga kumpeleka Hispania mwezi Desemba kwa safari inayolenga kumpa uzoefu wa soka.


Hatua hiyo inampa Nevada nafasi ya kuendelea kukuza kipaji chake licha ya tukio lililozua mjadala mkubwa ulimwenguni ,Kwa mtoto huyo, kuitiwa polisi uwanjani kunaweza kuwa tukio lililoanzisha safari mpya ya kutimiza ndoto yake ya soka.

Kila jambo linatokea kwa sababu , washukuliwe wazazi walioita polisi kwani bila wao kipaji Cha mtoto Nevada kisinge onekana , ila kwa sasa kipaji kimeonekana na mtoto kaanza ukurusa mwingine kwenye safari yake ya soka.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments