Kuelekea dabi ya kariakoo haya ni maboresho wakati na kabla ya mchezo


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mfumo mpya wa FVS utakaoanza kutumika katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga Oktoba 10, 2026, utalipa kila benchi la ufundi kadi mbili za kuomba mapitio ya maamuzi ya mwamuzi, Kanuni hiyo imetangazwa na CEO wa bodi ya ligi Cornel Barnabas.

Kwa mujibu wa mfumo huo, benchi litatumia kadi hiyo pale linapoona kuna tukio linalohitaji mwamuzi kwenda kupitia tukio hilo , endapo mwamuzi atakwenda kwenye FVS na kubaini kuwa benchi lilikuwa sahihi, kadi yake itaendelea kubaki.

Hata hivyo, iwapo mwamuzi ataenda kupitia tukio na kubaini kuwa uamuzi wake wa awali ulikuwa sahihi, benchi litapoteza kadi moja na kubaki na moja.

Benchi litakapokosea mara mbili na mwamuzi akathibitisha kuwa maamuzi yake yalikuwa sahihi, kadi zote mbili zitaondolewa, baada ya hapo, maamuzi yaliyobaki yatafanywa na mwamuzi bila ombi la benchi kurejea tukio. Iwapo Kuna tukio litakuwa na utata bas mwamuzi mwenyewe ataamua kwenda kuhakikisha licha ya timu fulani kutokuwa na nafasi, hivyo hata kama nafasi za kuomba marejeo zitakuwa zimeisha haimaanishi kuwa hatangalia, ila iwapo Kuna tukio tata mwamuzi anayo nafasi ya kufanya marejeo.

Mfumo huo unalenga kuweka utaratibu wa matumizi ya FVS wakati wa mchezo, huku ukilipa benchi nafasi ya kuomba mapitio pale linapoona kuna jambo linalohitaji kuangaliwa, jambo hili litafanya mabenchi ya ufundi kuongeza umakini wakati wa kuomba marejeo kwa kuhofia kupoteza nafasi.


Mbali na mfumo wa kadi, kumekuwa na malalamiko kuhusu hali ya hewa katika vyumba vya kubadilishia nguo, ambapo baadhi ya timu zimekuwa zikiepuka kutumia vyumba hivyo kutokana na matukio yanayohusishwa na matumizi ya dawa za hewa.

Katika kukabiliana na hilo, kifaa maalumu kitatumika kupima hali ya hewa ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo huku Madaktari wa timu zote mbili wakihusika katika zoezi hilo ili kuhakikisha hali ya hewa inakidhi mazingira yanayofaa kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Mfumo huo wa FVS pamoja na utaratibu wa kupima hali ya hewa unatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Simba na Yanga utakaochezwa Oktoba 10, 2026 katika dimba la Uhuru.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments