Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kila mafanikio huanza kama hatua na Kila jambo Lina mwanzo na mwisho wake ,Safari ya Cristiano Ronaldo kwenye kufumania nyavu kuelekea kufikisha mabao 1,000 katika soka la kulipwa ilianza Oktoba 7, 2002, alipofunga bao lake la kwanza akiwa na timu ya wakubwa ya Sporting CP ya Ureno na ndio ukawa mwanzo wa nyavu kupataateso kutoka kwa Ronaldo.
Siku ambayo nyota huyo anajitbulisha kwenye soka Sporting CP ilikuwa mwenyeji wa Moreirense katika mchezo wa ligi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambapo Ronaldo, aliyekuwa akianza kujijenga katika kikosi cha wakubwa, alifunga mabao mawili katika mchezo huo.
Kabla ya hapo, Ronaldo alikuwa amefunga katika ngazi za vijana, lakini mabao hayo hayahesabiwi kama bao lake la kwanza katika timu ya wakubwa.
Tangu siku hiyo, mshambuliaji huyo wa Ureno ameendelea kufunga akiwa na klabu mbalimbali alizochezea, zikiwemo Manchester United, Real Madrid, Juventus na Al Nassr, pamoja na timu ya taifa ya Ureno akiwa na Jumla ya mabao 980.
Hivyo, Oktoba 7, 2002, ni tarehe muhimu katika historia ya Ronaldo, kwani ndiyo siku aliyofungua akaunti yake ya mabao katika soka la wakubwa na kuanza safari iliyomfikisha karibu na alama ya mabao 1,000.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment