Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester City wamewasilisha rasmi rufaa dhidi ya uamuzi wa Tume Huru iliyowakuta na hatia ya kuvunja kanuni za kifedha za Ligi Kuu England (EPL).
City wamewasilisha rufaa hiyo wakisisitiza kuwa uamuzi huo una makosa ya kisheria, kanuni na ukweli, huku klabu hiyo ikiendelea kudai kuwa haina hatia.
Rufaa hiyo sasa itasikilizwa na Bodi Huru ya Rufaa, wakati suala la adhabu likiwa bado halijaamuliwa, miongoni mwa adhabu zinazoweza kuzingatiwa ni kukatwa alama,faini, zuio la usajili au kushushwa daraja.
Hata hivyo, adhabu ya kushushwa daraja kutoka EPL kutakuwa sehemu ya adhabu inayopendekezwa, hatima yao haitategemea tume huru pekee, kwani uamuzi huo unatakiwa kuridhiwa kwa kura ya vilabu vingine vya ligi.
Vilabu 19 vya EPL ndivyo vitakavyokuwa na nafasi ya kupiga kura, huku angalau vilabu 15 kati ya 19 vikihitajika kuunga mkono kushushwa kwa City ili hatua hiyo ipitishwe, endapo idadi hiyo haitapatikana, City hawatashushwa kwa kuzingatia utaratibu huo.
Kwa sasa, dalili zinaonyesha kuwa kupata kura hizo 15 si jambo rahisi kwa mujibu wa Sky Sports imeripoti kuwa viongozi wa klabu mbili za EPL wameeleza kuwa watashangaa iwapo vilabu 15 vitakubali kuishusha City, wakitaja pia athari za kibiashara ambazo uamuzi huo unaweza kuleta kwa ligi nzima.
Hata hivyo, bado hakuna kura iliyopigwa na hakuna uamuzi wa mwisho kuhusu hatima ya City, mchakato wa rufaa na usikilizwaji wa adhabu utaendelea kabla ya hatua hiyo kufikiwa.
Kwa upande mwingine, kukatwa pointi au kupewa faini hakuhitaji kura ya vilabu vya EPL, Kura hiyo inakuwa muhimu hasa iwapo adhabu ya kushushwa kwa City kutoka ligi kuu itawekwa mezani.
0767916/5473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment