Gyokeres aweka historia kufumania nyavu UEFA nations League


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Sweden, Viktor Gyökeres, ameweka historia katika michuano ya UEFA Nations League baada ya kufunga katika michezo sita mfululizo, rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji mwingine katika historia ya mashindano hayo.

Mfululizo huo ulianza Oktoba 2024 alipofunga dhidi ya Estonia, kabla ya kuendelea kufunga dhidi ya Slovakia na Azerbaijan, ambapo alifunga mabao manne katika mchezo mmoja.

Gyökeres aliendeleza mfululizo huo katika msimu wa 2026/27 kwa kufunga dhidi ya Romania, Poland na hatimaye Bosnia & Herzegovina, bao lililomuweka kwenye historia ya Nations League.


Kwa kufanya hivyo, amevunja rekodi ya michezo mitano mfululizo iliyokuwa ikishikiliwa na Aleksandar Mitrovic wa Serbia na Benjamin Sesko wa Slovenia.

Michezo aliyofunga mfululizo:

1.Estonia – bao moja

2. Slovakia – bao moja

3. Azerbaijan – mabao 4

4. Romania – bao moja

5. Poland – bao moja

6. osnia & Herzegovina – bao Moja.

Hivyo, Gyokeres sasa ndiye mchezaji wa kwanza kufunga katika michezo sita mfululizo ya Nations League.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments