Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hatima ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kati ya Morocco na Senegal inaweza kuchukua sura mpya baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (TAS/CAS) kupanga kusikiliza kesi hiyo kesho, Oktoba 8, 2026.
Kesi hiyo iliwasilishwa na Senegal ikipinga uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3-0, licha ya Senegal kushinda fainali hiyo kwa bao 1-0 baada ya muda wa nyongeza.
Senegal inataka uamuzi wa CAF ubatilishwe na ushindi wa 1-0 uliopatikana uwanjani utambuliwe, wakati Morocco inaendelea kusimamia uamuzi uliotolewa na CAF.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, TAS itaanza mchakato wa kufikia uamuzi, huku tarehe rasmi ya kutolewa kwa hukumu ikiwa bado haijawekwa wazi.
Kwa hiyo, kusikilizwa kwa kesi hiyo kunafungua tena mjadala wa nani anapaswa kutambuliwa kama bingwa wa AFCON 2025, huku uamuzi wa TAS ukisubiriwa kuhitimisha suala hilo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment