Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva, amebakiza bao moja kuvunja rekodi ya Mrisho Ngassa na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya Taifa.
Msuva hadi sasa amefunga mabao 25 akiwa sawa na Ngassa, ambaye tayari amestaafu soka hivyo, bao moja pekee linamtenganisha Msuva na rekodi hiyo ambayo inaweza kumfanya kuandika historia mpya katika soka la Tanzania.
Ilitarajiwa Msuva angefikia au kuvunja rekodi hiyo katika michezo ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar, hata hivyo, mshambuliaji huyo hakufanikiwa kufumania nyavu katika michezo hiyo, hivyo rekodi bado imeendelea kubaki kuwa sawa kwa wachezaji hao wawili.
Sasa macho yanaelekezwa kwenye michezo ijayo ya Taifa Stars, ambapo Msuva anahitaji bao moja pekee kumzidi Ngassa na kuchukua nafasi ya juu kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa timu ya Taifa.
Kwa Msuva, bao hilo si tu litaongeza idadi yake ya mabao, bali pia litamweka katika historia ya Taifa Stars kama mfungaji anayeongoza kwa mabao mengi zaidi.
Wafungaji bora muda wote Taifa stars.
Simon Msuva 25
Mrisho Ngassa. 25
Mbwana Samatta 22
John Bocco 16.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment