Afcon imeshindwa kwenda kama kombe la Dunia


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefanya mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), baada ya kubadili uamuzi wake wa awali wa kufanya mashindano hayo kila baada ya miaka minne.

Awali, CAF ilikuwa imepanga kuanzia baada ya toleo la mwaka 2028, AFCON iwe inafanyika kila baada ya miaka minne badala ya utaratibu wa sasa wa kila baada ya miaka miwili, mabadiliko hayo yalilenga kuoanisha kalenda ya mashindano ya Afrika na ratiba ya kimataifa ya soka.

Hata hivyo, katika uamuzi mpya uliofanyika Oktoba 29, 2026, CAF imeamua kurejesha mfumo wa AFCON kufanyika kila baada ya miaka miwili, hatua inayomaanisha kuwa mashindano hayo yataendelea kuchezwa kwa utaratibu uliozoeleka kwa mataifa ya Afrika.

Uamuzi huo unakuja wakati ambao CAF inaendelea kufanya marekebisho katika kalenda ya mashindano yake, huku ikizingatia maslahi ya vyama vya soka, timu za taifa na wadau wengine wa mchezo huo.

Mabadiliko hayo yanaonesha kuwa CAF imeamua kuendelea na mfumo wa miaka miwili, huku AFCON ikiendelea kuwa mashindano makubwa ya soka la timu za taifa barani Afrika.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments