Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester City imekabiliwa na jumla ya tuhuma 115 zinazohusiana na ukiukaji wa kanuni za Ligi Kuu England, huku sehemu kubwa ya tuhuma hizo zikihusu taarifa za kifedha za klabu.
Tuhuma hizo zinahusu kipindi cha kuanzia msimu wa 2009/10 hadi 2022/23, huku Manchester City ikiendelea kupinga makosa hayo, Wadau na wapenzi wa soka wamekuwa wakisikia klabu ikikabiliwa na makosa lakini wanashindwa kuelewa mtiririko mzima wa makosa hayo.
Hizi ni tuhuma ambazo klabu inakabiliwa nazo.
Kati ya tuhuma hizo, 54 zinahusu madai ya kushindwa kutoa taarifa sahihi za kifedha kwa Premier League katika kipindi cha 2009/10 hadi 2017/18.
Tuhuma nyingine 14 kuhusu malipo ya wachezaji na makocha, wakati tano zinahusisha ukiukaji wa kanuni za UEFA, ikiwemo masuala ya Financial Fair Play.
Aidha, City inakabiliwa na tuhuma saba zinazohusu kanuni za Premier League za Profitability and Sustainability Rules (PSR).
Tuhuma 35 zilizobaki zinahusu madai ya klabu kushindwa kushirikiana kikamilifu na Premier League katika uchunguzi uliofanyika kuanzia mwaka 2018 hadi 2023.
Kwa ujumla, tuhuma hizo zinagawanyika katika makundi hayo matano, huku suala hilo likiwa na uzito kutokana na kipindi kinachohusisha baadhi ya miaka ambayo City ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Manchester City imekuwa ikikanusha tuhuma hizo na kusisitiza kuwa ina ushahidi wa kujitetea dhidi ya madai yanayoikabili.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment