Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Nyota wa Sunderland na nahodha wa timu ya taifa ya Uswisi, Granit Xhaka, amekiri kutumia cheti bandia cha chanjo ya COVID-19 mwaka 2022, jambo lililosababisha kuanza kwa uchunguzi dhidi yake nchini Uswisi.
Nyota huyo amesema kuwa wakati huo alikuwa na hofu na mashaka kuhusu chanjo hiyo, lakini sasa amekiri uamuzi wa kutumia cheti hicho ulikuwa kosa na ameomba msamaha.
Kutokana na suala hilo, Xhaka amekubaliana na Shirikisho la Soka la Uswisi kutoshiriki katika kambi ya sasa ya timu ya taifa wakati uchunguzi dhidi yake ukiendelea, Shirikisho hilo limesema litapitia hali yake tena baada ya michezo ya kimataifa.
Mamlaka za Uswisi zinaendelea kuchunguza kama matumizi ya cheti hicho yalihusisha kosa la jinai huku Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, makosa yanayohusisha kughushi nyaraka nchini Uswisi yanaweza kuwa na adhabu ya hadi miaka mitano ya kifungo au faini kubwa , japo kuwa hatua yoyote dhidi ya Xhaka itategemea matokeo ya uchunguzi ambapo tayali binafsi amekiri.
Xhaka amesema yuko tayari kushirikiana na mamlaka katika mchakato huo, huku akiwa bado anachukuliwa kuwa hana hatia hadi uamuzi wa kisheria utakapofikiwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment