Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kwa miaka ya nyuma, ilikuwa nadra kusikia mwamuzi kutoka Tanzania akipewa jukumu la kuchezesha michezo ya mashindano makubwa barani Afrika lakini Sasa hali imeanza kubadilika, huku waamuzi wa Tanzania wakipewa nafasi katika michezo ya CAF.
Hatua hiyo inaonekana baada ya CAF kuwateua waamuzi wanne kutoka Tanzania kusimamia mchezo wa Klabu Bingwa Afrika utakao wakutanisha JS Saoura ya Algeria na Horoya AC ya Guinea, utakaochezwa Septemba 4, 2026 katika Uwanja wa Miloud Hadefi, Algeria.
Ahmed Arajiga ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Nasir Salum na Mohamed Mkono, huku Ally Ramadhani akipewa jukumu la mwamuzi wa VAR.
Uteuzi wa waamuzi hao unaongeza mwendelezo wa ushiriki wa waamuzi wa Tanzania katika mashindano ya CAF, baada ya kupata nafasi katika michezo mbalimbali ya kimataifa na Imani dhidi Yao inazidi kukua ikichagizwa na maendeleo ya soka nchini.
Mabadiliko hayo yanaonyesha kuwa waamuzi wa Tanzania wameendelea kupata uzoefu kupitia michezo ya ndani , jambo linalowapa nafasi ya kuaminiwa katika mashindano yanayosimamiwa na CAF.
Kutoka katika kipindi ambacho uteuzi wa mwamuzi wa Tanzania katika mechi za CAF ulikuwa jambo lisilo la kawaida, sasa majina ya waamuzi hao yanaendelea kuonekana katika uteuzi wa michezo mbali mbali ya kimataifa.
Mchezo wa JS Saoura dhidi ya Horoya AC utakuwa nafasi nyingine kwa waamuzi hao kuendelea kujenga uzoefu, imani na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya soka barani Afrika.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment