United kutwaa ubingwa wa EPL 2017/18


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Manchester United inaweza kukabidhiwa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2017/18 endapo Manchester City itapokonywa taji hilo kutokana na kesi inayohusu ukiukwaji wa kanuni za Premier League kwenye masuala ya kifedha

City inakabiliwa na mashitaka 115 yanayohusiana na masuala ya fedha, ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, imepatikana na hatia katika makosa 114, Hata hivyo, suala hilo bado linaendelea katika hatua za kisheria na City ina nafasi ya kukata rufaa.

Msimu wa 2017/18, Manchester City ilimaliza kileleni ikiwa na alama 100 na kutwaa ubingwa, huku Manchester United ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 81.

Endapo moja ya adhabu itakayotolewa kwa City itakuwa ni kupokonywa ubingwa wa misimu sita waliyotwaa suala litakalofuata ni kupewa ubingwa kwa timu iliyomaliza nafasi ya pili.

Hata hivyo bado uamuzi wa mwisho haujafikiwa na adhabu haijatolewa huku City wakiwa na nafasi ya kujitetea kupitia rufaa.

Iwapo utaratibu huo utatumika , timu zilizomaliza nafasi ya pili katika misimu ambayo City ilitwaa ubingwa, ikiwemo Liverpool na Arsenal, pia zitaingia kwenye mjadala wa kugawiwa mataji hayo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments