Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Teknolojia imeingia katika soka kwa lengo la kusaidia waamuzi kufanya maamuzi sahihi na kuondoa utata kwenye baadhi ya matukio kwa kufanya marejeo, lakini tukio la Manchester Derby limeonyesha kuwa bado haiwezi kuwa jibu la mwisho katika kila uamuzi.
Katika mchezo wa Manchester United dhidi ya Manchester City uliochezwa Old Trafford septemba 13, 2026 bao la Erling Haaland lilizua mjadala baada ya Pro Ref kufanya mapitio na kueleza kuwa kulikuwa na kosa katika uamuzi wa kuruhusu bao hilo, huku VAR ikishindwa kubaini athari ya nafasi ya Enzo Fernandez katika tukio hilo.
Hali hii inatukumbusha kuwa teknolojia haiwezi kuondoa kabisa makosa ya kibinadamu bali Inatumika na binadamu ambao nao wanaweza kuona tukio moja kwa namna tofauti kutokana na tafsiri, hisia au mtazamo wao. Hata hivyo, baada ya mapitio, uamuzi unaweza kubainika kuwa haukuwa sahihi au sahihi.
Kwa mantiki hiyo, wadau na mashabiki wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanapaswa kuiona FVS kama chombo cha kupunguza makosa, si kuyamaliza. Teknolojia inaweza kusaidia kubaini matukio ambayo macho ya mwamuzi yameshindwa kuyaona, lakini bado uamuzi wa mwisho unahitaji binadamu ambaye ni muamuzi kuamua.
Kinachotakiwa ni kuhakikisha makosa yanayoweza kubadilisha matokeo ya mchezo, hasa yale yanayogharimu timu kupata alama, yanatakiwa kuangaliwa kwa umakini zaidi.
Manchester Derby imetoa mfano wa jambo hilo, ambapo Manchester United imejikuta ikikosa alama tatu, na matokeo kama haya yanaweza kuwa na athari katika msimamo wa ligi kadri msimu unavyoendelea.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment