Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amesema mshambuliaji wa klabu hiyo Julian Alvarez atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo baada ya kumalizika kwa sakata lililomhusu mchezaji huyo katika kipindi cha majira ya joto.
Ikumbukwe kuwa Alvarez aliingia kwenye mgogoro na mashabiki wa Atletico baada ya kuonyesha nia ya kujiunga Fc Barcelona jambo ambalo liliwafanya mashabiki wa klabu hiyo kumzomea nakutengeza hali ya sintofahamu baina ya mchezaji na mashabiki wa klabu hiyo.
Hata hivyo Simeone amesema kuwa Alvarez amekuwa akifanya mazoezi vizuri na sasa anatarajiwa kuendelea kuitumikia Atletico Madrid pamoja na wachezaji wenzake.
“Julian Alvarez atakuwa kwenye kikosi, anafanya mazoezi vizuri na sote tunatarajia kufanya vizuri kutoka kwake, kama tunavyotarajia kutoka kwa wachezaji wenzake,” alisema Simeone.
Kocha huyo pia amesema Alvarez anapaswa kuangalia mbele na kutumia nafasi aliyonayo ndani ya Atletico, akisisitiza kuwa maisha yana fursa nyingi kwa wachezaji.
Kocha huyo aliongeza kuwa sakata lililomhusisha Alvarez linaweza kuwa sehemu ya mafunzo kwake, huku akisisitiza umuhimu wa kupunguza tabia ya kuhukumu na badala yake kujifunza kutokana na yaliyotokea.
“Mara nyingi tunatumia maisha yetu kuwahukumu wengine, tunahitaji kufanya hivyo kidogo na kujifunza zaidi, Natumaini hili limekuwa tukio la kujifunza kwake baada ya majira haya ya joto,” aliongeza Simeone.
Simeone amemalizia kwa kumtakia Alvarez kuwa na furaha akiwa Atletico Madrid na kuonyesha hilo kupitia uwanjani kwa kufunga mabao.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment