Siku 701, United bila kulipa deni la shabiki


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Manchester United huenda ikawa imeanza msimu mpya ikifikiria kusaka matokeo na kujenga timu, lakini kuna jambo jingine ambalo wachezaji wake wanapaswa kulikumbuka ni kuna shabiki anayesubiri miguu yao itimize nadhiri yake.

Frank Ilett, alianza changamoto ya kutokata nywele zake hadi Manchester United ishinde michezo mitano mfululizo na Sasa changamoto hiyo imefika siku ya 701, huku nywele zake zikiendelea kukua kutokana na United kushindwa kufikisha ushindi huo wa michezo mitano mfululizo.


Ilett ameifanya changamoto hiyo kuwa sehemu ya safari yake ya kuishabikia United kupitia ukurasa unaojulikana kama The United Strand. Kila ushindi wa United humsogeza hatua moja karibu na siku ya kukata nywele, wakati matokeo yasiyoruhusu mfululizo wa ushindi humrudisha kuanza mwanzo.

Msimu wa 2026/27 umeanza, lakini United haijaanza kwa mwendo ambao ungemsaidia Ilett kukamilisha nadhiri yake, Katika michezo mitatu ya mwanzo, United imeshinda mmoja, imetoka sare mmoja na imepoteza mmoja. Mchezo wa mwisho dhidi ya Everton ulimalizika kwa sare ya 2-2, matokeo ambayo yamekatiza mfululizo wa ushindi nakumfanya shabiki huyo kuanza mah sabu upya.

Miguu ya United ndiyo jibu ,hapa ndipo wachezaji wa United wanapoweza kukumbushwa kuwa nyuma ya matokeo yao kuna shabiki anayesubiri hatima yake , Ilett amefikisha siku 701 bila kukata nywele kwa sababu ya timu anayoiunga mkono kushindwa kustahimili matokeo mazuri. Sasa ni miguu ya wachezaji ndiyo inaweza kubadilisha safari hiyo kutoka kuwa changamoto inayoendelea hadi kuwa siku ya kusherehekea.


Kwa klabu yenye historia kama Manchester United, kushindwa kupata ushindi wa michezo mitano mfululizo si jambo ambalo mashabiki wangependa kuliona likiendelea kuwa kawaida. Na kwa Ilett, hilo lina maana zaidi kwa sababu kila sare au kipigo kinaongeza siku nyingine kwenye nadhiri yake.

Hivyo, msimu huu United inapambana kwa ajili ya alama, nafasi kwenye msimamo na mafanikio ya timu. Lakini wakati huo huo, Frank Ilett anasubiri ushindi mwingine mmoja baada ya mwingine ili kukamilisha ahadi aliyo ahidi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments