Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Usajili wa Enzo Fernandez kutoka Chelsea kwenda Manchester City kwa ada ya euro milioni 145 umeongeza jina jipya kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi zaidi katika historia ya soka.
Fernandez, ambaye amejiunga na Manchester City katika dirisha la msimu wa 2026/27, sasa anashika nafasi ya tatu kwa pamoja na Alexander Isak kwa kuzingatia ada ya uhamisho.
Orodha hiyo inaongozwa na Neymar, aliyesajiliwa na Paris Saint-Germain kutoka Barcelona mwaka 2017 kwa euro milioni 222, Uhamisho huo bado unaongoza kwenye rekodi ya ada kubwa zaidi kuwahi kulipwa kwa mchezaji.
Kylian Mbappe anashika nafasi ya pili baada ya kuhamia PSG kutoka Monaco mwaka 2018 kwa euro milioni 180.
Nafasi ya tatu inashikiliwa kwa pamoja na Fernández na Isak, Fernandez amehamia Manchester City akitokea Chelsea mwaka 2026, wakati Isak alihama Newcastle United kwenda Liverpool mwaka 2025, kwa ada inayofikia euro milioni 145.
Morgan Rogers anakamilisha tano bora baada ya kuhamia Chelsea kutoka Aston Villa katika dirisha la 2026/27 kwa ada ya takriban euro milioni 138.
Kwa mpangilio wa ada, orodha hiyo inakuwa Neymar (€222m), Mbappe (€180m), Fernandez (€145m), Isak (€145m) na Rogers (€138m).
Usajili wa Fernandez na Rogers katika dirisha la msimu huu umeongeza mabadiliko kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kuhamishwa kwa ada kubwa katika soka la Ulaya.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment