Ronaldo, Messi wabakia na heshima UEFA, Mbappe afukizia kuvunja historia


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika ulimwengu wa soka, rekodi huacha alama kwa muda mrefu, lakini kizazi kipya huja na nafasi ya kuandika historia upya, Hivyo ndivyo ilivyo katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, UEFA Champions League.

Cristiano Ronaldo bado anaongoza orodha hiyo akiwa na mabao 141, akifuatiwa na Lionel Messi mwenye mabao 129, Wawili hao wameweka kiwango ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kipimo kwa washambuliaji wanaokuja nyuma yao.

Nyuma yao yupo Robert Lewandowski mwenye mabao 109, huku Karim Benzema akiwa na 90. Raul anashika nafasi ya tano kwa mabao 71, akilingana na Kylian Mbappe ambaye pia amefikisha idadi hiyo.

Tofauti kubwa kwa Mbappe ni umri na muda ambao bado anao mbele yake katika mashindano hayo, Wakati Ronaldo na Messi wakielekea mwisho wa safari zao za soka, Mbappe bado ana nafasi ya kuongeza idadi hiyo msimu baada ya msimu.

Kwa sasa, Mbappe anahitaji mabao 71 zaidi ili kufikia 142 na kumpita Ronaldo kama mfungaji bora wa muda wote wa Champions League.

Swali linalobaki ni kama Mbappe ataweza kuendeleza kasi hiyo na kufikia rekodi iliyowekwa na Ronaldo, tayari ameshawahi kuonyesha uwezo wa kuvunja rekodi ya ufungaji Bora wa muda wote kombe la Dunia iliyokuwa ikishiliwa na Messi, jambo linalofanya mbio zake za kuelekea kileleni mwa orodha hii kuwa sehemu nyingine ya historia inayosubiri kuandikwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments